Sitakaa Kimya Tena – Madam Flora
Msanii wa nyimbo za injili nchini Madam Flora ambaye aliwahi kuwa mke wa muimbaji injili Emmanuel Mbasha amefunguka na kusema sasa hivi hata kaa kimya kwa watu wote ambao wanakuwa wakimzushia habari mbalimbali.
Madam Flora amesema hayo kupitia ukurasa wake wa Instagram baada ya chombo kimoja cha habari kusambaza habari kuwa ameachana na aliyekuwa mume wake kutokana na kutoridhishwa kimapenzi na mtu huyo habari ambayo ilikuwa ikisomeka ” Flora Mbasha : Hakuna haja ya kuwa na mwanaume asiyekuridhisha kinyumba” jambo ambalo amelikana na kusema yeye hajazungumza maneno hayo.
“Hizi habari ni za uongo, sijafanya mahojiano na radio yoyote na kuzungumza maneno hayo kama ilivyo sambaa mitandaoni. Naomba mzipuuze maana ni mpuuzi mmoja tu ameamua kuonyesha upuuzi wake na kutafuta ‘followers’ kwenye page yake. Na niseme tu kwamba hivi sasa sitakaa kimya tena, huyo aliyezoea kunizushia story za uongo akifikiri siijui sheria ajipange vizuri maana mahakama ipo na sheria ipo” alisisitiza Madam Flora
Madam Flora ambaye sasa ni mke halali wa Daud Kusekwa ametoa kitabu chake alichokipa jina la ‘Siri za Flora Mbasha’ ambacho kinaelezea maisha yake na yale aliyopitia katika ndoa kabla ya kujivua minyororo na kutoka katika maisha ya Emmanuel Mbasha na kuingia katika ndoa nyingine na Mr Daud.