-->

Mashauzi Yanapoteza Wasanii Wengi-Diamond Platnumz

Msanii Diamond Platnumz amefunguka na kusema wasanii wengi wa Tanzania na Afrika Mashariki kiujumla wanapotea kwenye ramani ya muziki sababu kubwa ni mashauzi na starehe na kutaka kujionesha.

diamond32

Akizungumza kwenye kipindi cha Planet Bongo kinachorushwa na East Africa Radio, Diamond Platnumz amedai kuwa mafanikio yake kimuziki na kuzidi kuendelea kufanya vizuri ni kutokana na ukweli kwamba yeye si mtu wa starehe na wala si mtu wa mashauzi kutaka kufanya vitu ili kuwaonesha watu, bali yeye amekuwa akitunza pesa anazofanya na kufanya mambo ya msingi ndiyo maana labda anazidi kufanikiwa kimaisha pamoja na sanaa.

“Unajua wasanii wengi wanapoteza na kushuka kimuziki sababu ya starehe pamoja na mashauzi, unakuta mtu amepata mafanikio kidogo anaanza mashauzi na kufanya starehe zisizo na tija, ndiyo maana mimi huwezi kuniona kwenye starehe hata wasanii wa WCB ni hivyo hivyo” alisema Diamond Platnumz.

Katika hatua nyingine Diamond Platnumz amemwelezea msanii Shettah na kusema ni mfano mzuri kwani Shettah na yeye wanazijua pesa hivyo ni wabahili sana wanaweza kutoka kufanya show na ukiwapiga kizinga cha pesa watakwambia kuwa hawana pesa.

‘Mimi namkubali sana Shettah kwani jamaa ni bahili sana anaweza kutoka kufanya show na akakwambia sina pesa, hata gari yake aliyonunua juzi amenunua kwa pesa zake sababu anakusanya pesa zake na kufanyia vitu vya msingi, saizi Shettah anajenga nyumba yake na hiyo yote sababu si mtu wa mashauzi na wala si mtu wa starehe” Alisema Diamond Platnumz

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364