Picha: Lady Jaydee Arudisha ‘Ubinti’ na ‘Urnb’ Kwenye Wimbo Mpya ‘Ndindindi’
Lady Jaydee ameamua kuvua gamba na kurudi upya kama binti wa miaka 10 iliyopita na kurejesha ladha aliyoanza nayo na iliyompa umalkia, R&B.
Lady Jaydee akisaini mkataba na Mkito ambako wimbo wake utapatikana. Kushoto ni mwakilishi wa kampuni hiyo, Aishi
Muimbaji huyo mkongwe amefanya uzinduzi wa single yake mpya aliyoipa jina ‘Ndindindi’ Jumamosi hii pale Sky Nightlife, Masaki jijini Dar es Salaam baada ya kuendesha kampeni ya mwezi mzima ya ujio wake mpya, #NaamkaTena.
Mwakilishi wa Mkito, Aishi akisaini mkataba
Akiongea nasi, Jide amesema ameamua kuja na ladha hiyo kwakuwa hakutaka kutabirika.
“Kila siku hautakiwi kuwa mtu ambaye unatabirika. Sanaa ni ubunifu, ukifanya kitu kile kile kila siku watu wanachoka kwahiyo inabidi uwe unabadilika ili watu wasikuzoee kila siku,” amesema.
Mshindi wa tatu wa Miss Tanzania 2014, Jihand kushoto alihudhuria pia uzinduzi wa single hiyo
Amesema Ndindindi ni wimbo alioshirikiana kuuandika na Terrence Mwakaliku pamoja na msanii wa Uganda, Naava.
Wimbo huo umetayarishwa jijini Kampala Uganda na Andy Music na utapatikana kwenye album yake ya saba iitwayo Woman.
Amedai kuwa Woman itakuwa ni album yenye mchanganyiko wa ladha na ambayo itaweza kufit kila rika.
Lady Jaydee na mtangazaji wa Times FM, Lil Ommy
Chanzo: Bongo5