-->

Masogange Kuletewa Mashahidi Watatu

BAADA ya msanii na mnogeshaji wa video za wasanii mbalimbali, Agnes Gerald (Masogange), kuikana ripoti ya mkemia mkuu wa Serikali iliyoonyesha kwamba Februari 20, mwaka huu ilithibitisha mkojo wake kuwa na dawa za kulevya aina ya heroin na Oxazepam, upande wa mashtaka unatarajia kuleta mashahidi watatu kwenye kesi hiyo.

Akisoma maelezo ya awali katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, mbele ya Hakimu Mkazi, Wilbard Mashauri, Wakili wa Serikali, Constantine Kakula, alidai upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na kuiomba mahakama hiyo kuwasilisha mashahidi kwa ajili ya kutoa ushahidi wao.

Alidai mshtakiwa huyo alikamatwa Februari 14 nyumbani kwake na kupelekwa kituo cha kati cha polisi kwa ajili ya kuhojiwa na Februari 15 alipelekwa kwa mkemia mkuu kwa ajili ya kupimwa mkojo.

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364