-->

Ray Kigosi Alia na Yanga, ‘Tumuombe Manji Arudi’

Muigizaji wa Filamu nchini, Ray Kigosi amesema uongozi wa klabu ya Yanga ni vema ukafanya utaratibu wa kamrejesha aliyekuwa Mwenyekiti wao, Yusuph Manji ili timu hiyo iwezi kupata maandalizi mazuri kwa ajili ya msimu ujao wa ligi na kusajili wachezaji wazuri ili wafanye vizuri katika mashindano ya kimataifa.

Kupitia mtandao wa instagram Ray amendika, “Nakumbuka kipindi kama hiki cha matayarisho ya msimu mpya tumezoea kuona timu yetu ikipelekwa Ulaya kujiandaa, ikitumia mamilioni ya fedha kwenye maandalizi ya usajili. Nakumbuka timu yetu ilitoka kucheza mechi ya kimataifa, Makamu Mwenyekiti ‘Sanga’ alirudi na mamilioni ya fedha ambayo ni chenji iliyobaki, yaani hesabu zinazidi makadirio ya timu yetu , je ni nani zaidi ya Manji aliyetupa furaha hizi?.

“Viongozi wangu Manji tunamuhitaji sana kwenye klabu yetu, tumpeni timu tupate raha duniani, tusajili wachezaji wenye focus ya mashindano ya kimataifa si ligi ya hapa ubingwa mara tatu mfululizo tumebakiza nini tena?. Sisi wanachama na mashabiki ndio tunaoumia  zaidi yenu viongozi, sisi hulipa viingilio uwanjani, je ni kiongozi gani hulipa kiingilio?,  sisi hulipia kadi zetu kwa jasho wakati viongozi ulipwa mishahara na posho pia, ni shabiki gani analipwa posho na mshahara,” ameendelea kuongeza.

“Mpira pesa sio kukaa pale Jangwani na kucheza bao, Yanga yetu ndio mkombozi wetu, tumuombe Manji arudi kwa nguvu sote ili arudishe furaha yetu, tusipoziba ufa tutajenga ukuta, ni mawazo yangu kwa timu yangu, Yanga Daima mbele nyuma mwiko”  ameandika Ray.

Bongo5

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364