-->

Mastaa Wasusia Harusi ya Beka

Jana ilikuwa ni siku ya sherehe ya ndoa ya msanii wa filamu Bongo, Bakari Makuka ‘Beka’ ambapo ilifana vilivyo huku waalikwa wakila, kunywa na kuserebuka vilivyo.

Sherehe hiyo ilifanyika katika Ukumbi wa Prime Rose uliopo Mbezi Beach, Dar ikiwa ni baada ya kufunga ndoa na mkewe Nasra, Ijumaa iliyopita katika msikiti wa Ununio, Jumamosi ikafuatiwa na sherehe ya Maulid nyumbani kwao Beka, Sinza, Dar.

harusi-ya-becka-10

Beka Akiwa na Mkewe Nasra

Katika sherehe hiyo mastaa wenzake ni kama walisusia kwani aliyekuwepo ni Kulwa Kikumba ‘Dude’ ambaye alikuwa bestman na Dk. Cheni ambaye alikuwa mshehereshaji jambo ambalo liliwashangaza baadhi ya wageni waalikwa kwani siyo kawaida ya wasanii kutotokea kwenye shughuli kama hiyo.

Alipoulizwa kuhusiana na hilo kwa nini wasanii wenzake hawakujitokeza, Beka alisema;

“Kiukweli hata mimi nashangaa maana nimewaalika wasanii wote lakini hawajaja sijui kwa nini.”

harusi-ya-becka-12

MC wa sherehe hiyo, Dk. Cheni akiwa kazini.

Maharusi pamoja na wanakamati wakipozi wakati wa harusi hiyo.

Maharusi pamoja na wanakamati wakipozi wakati wa harusi hiyo.

harusi-ya-becka-9

harusi-ya-becka-4

Kulwa Kikumba ‘Dude’ ambaye alikuwa bestman (kushoto) katika pozi na bibi harusi.

harusi-ya-becka-8 harusi-ya-becka-5

harusi-ya-becka-13

Maharusi wakitoka ukumbini baada ya shughuli.

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364