-->

Master Jay Atoboa Sababu za Yeye Kuoa Mapema

Mtayarishaji wa muziki mkongwe na mmiliki wa Studio ya Mj Records, Master Jay amefunguka na kusema kuwa yeye aliwahi kuoa mapema kutokana na ‘presha’ (shinikizo) la wazazi wake na jamii kiujumla.

Mkasi

Akizungumza kwenye kipindi cha Mkasi kinachorushwa na EATV, Master Jay amesema aliweza kumuoa mke wake wa kwanza akiwa mdogo kutokana na wazazi wake na kudai kuwa licha ya wao kuachana lakini mzazi mwenzake huyo ni bonge la mwanamke kwani anatabia njema na roho ya upendo sema ilifika mahali moyo wake uligoma tu lakini hakuwa na ubaya wowote ule.

Unajua wazazi wanakuwa wameshakupeleka shule baada ya hapo nilipomaliza, nikaanzisha biashara, ndiyo hapo wakaanza ohh miaka inaenda sijui nini na nini, yaani kuna vitu vingine tunapewa presha fulani hivi hivyo unajikuta unalazimisha vitu ili viwe vile ambavyo wao wanataka, hivyo hata mimi ilikuwa ni presha. Lakini sijutii kwani kutokana na ndoa yangu hiyo ya kwanza walitoka watoto wangu watatu ambao nawapenda sana,” alisema Master Jay.

Mbali na hilo Master Jay ameeleza kuwa hakulazimishwa kumuoa mwanamke huyo wala hakuletewa bali alimpenda mwenyewe na yeye ndiye aliyempeleka nyumbani kwao na kudai kuwa mpaka leo yule mwanamke ni bonge la mtu sababu anajiheshimu sana na anasifa zote sema ni vile moyo wake ulipishana naye.

Master Jay

eatv.tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364