-->

Matatizo Yamemfunza – Shamsa Ford

Msanii wa filamu nchini Shamsa Ford ambaye siku za karibuni muwewe alipatwa na maswahibu na kujikuta chini ya mikono ya polisi kwa tuhuma za kujihusisha na matumizi au kufanya biashara ya madawa ya kulevya.

Msanii wa filamu nchini, Shamsa Ford

Inawezekana kufuatia matatizo aliyopata muwe wake, Shamsa Ford amepata kujifunza kuwa siku zote watu ambao wewe unaweza kuwaona ni marafiki wakawa ndiyo maadui wakubwa katika maisha yako. Shamsa Ford anasema muda mwingine inawezekana mtu ambaye huna hata muda naye pengine ndiye mwema kwako kuliko hao unaokuwa nao karibu kila wakati.

“Mtu anayekupenda na mwema kwako ni ngumu kumjua, ukute hata huwa hakuongeleshi na hana time na wewe. Ila ukipatwa na shida ndo utamjua ila wale ambao kutwaa uko nao, unacheka nao, unawaamini hao ndiyo maadui zako wa kwanza. Ukidondoka kimaisha au mkigombana kidogo ndiyo wa kwanza kutangaza siri zako, kuwa makini na binadamu kwani binadamu wa sasa hata usipomkosea atakuadhibu tu” aliandika Shamsa Ford

eatv.tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364