-->

Steve Nyerere Aongea na Wanahabari, Amkaanga Wema Sepetu na Mama Yake (VIDEO)

Msanii wa filamu nchini Steven Mengele a.k.a Steve Nyerere amefanya mkutano na waandishi wa habari kwenye Ukumbi wa Millenium Tower, Makumbusho jijini dar es Salaam.

Steve Nyerere: Naomba radhi kwa watu wote ambaye nimewataja mule ndani kwenye ile sauti iliyosambaa kwenye Mitandao ya Kijamii(audio), nilifanya kwa kulinda chama changu na sikutaka dada yangu aniache. Nia ilikuwa kufanya binti huyu asitoke ndani ya CCM sababu ni pengo kwangu, Nliombe radhi bunge na Spika Ndungai kwa kauli nilizosema nmeshinikiza bunge

Steve Nyerere: Nlifanya kwa sababu sikutaka wema atoke ndani ya CCM Sina uwezo wa kuwashawishi wabunge.

Steve Nyerere: Nichukue nafasi hii kwa kumuomba msamaha rais Magufuli kwa kuwahusisha Wabunge aliowaamini kwenye Sakata hili. Naomba radhi Chama changu CCM kwa hili nliteleza.

Steve Nyerere: Napiga Magoti na kutubu kwa Mwenyezi Mungu.

Steve Nyerere: Nawaomba radhi ndugu wanahabari kwa kupoteza muda kufuatilia hili Jambo.

Steve Nyerere: Nia yangu ilikuwa kuhakikisha Wema hatoki ndani ya CCM.

Steve Nyerere: Ile audio ina siku tano nmeongea, baada ya kuiachia wakahama, labda walidhani tutahama wote. Mimi ntakuwa wa mwisho kuhama ndani ya CCM. Katika mkataba tulioingia na Chama Cha Mapinduzi hakuna sehemu mkataba huo unasema ukikamatwa na madawa ya kulevya, bangi kuwa chama hicho kitakuja kukusaidia

Steve Nyerere: Walifanya vile kunichafua na kuchafua Viongozi nlowataja. Kwanini nrekodiwe? Ni mambo gani mabaya nmewafanyia hadi wanirekodi, Nmetaja viongozi wa nchi wanaoaminika ndani ya nchi unaichukua audio ile unaitawanya.

Steve Nyerere: Wewe ni muuaji unataka kuniharibia maisha. Mama alichokifanya ni uuaji.

Steve Nyerere: Ningeanza kuongea matusi leo ningekuwa wapi?. Imeniuma. Walitaka kunigombanisha na Marafiki. Nmetafuta jina la kuniingizia liziki unakuja kunichafua. Nmemwamin sana Mama, nina meseji kibao amenijibu yeye amefanya unatakaje?

Steve Nyerere: Napita katika kipindi kigumu sana. Nlifanya ili kumkumbatia Wema.

Steve Nyerere: Yale yalikuwa Maongezi binafsi, yule ni mama mzazi, akiisikiliza ile audio anajisikiaje?

Steve Nyerere: Alijitokeza Mh Nape kuitetea Brand. Hii brand ninayoharibiwa leo ndo inaniweka Mjini.

Steve Nyerere: Jina hili nmelitafuta nmelipata, lisiniadhibu kupitia Mtu mwingine. Mama amenikosea sana, namwachia Mungu kwa kila Jambo. Naomba radhi kwa wale wote nliowataja. Wale wote nlowataja nliwasingizia, sikwenda kwa Nape wala Kwa nani. Nlikuwa nadanganya tu ili kuhakikisha Wema anakaa ndani ya CHAMA.

Swali; Wewe na Mkuu wa Mkoa mnaelewana?

Steve Nyerere: Kwenye maongezi yale kila kitu ni cha uongo. Hakuna ndugu wanaogombana. Nlisema vile sikuwa na jinsi, ilikuwa ili kumlidhisha Mama. Mimi na Mako sina Ugomvi naye kila siku tunashirikiana kurudisha hawa wanaopotea. Naungana na Mako kupiga vita haya mambo ya Madawa ya kulevya. Nawaomba radhi kwa wote nliyowataja.

Swali: Nini kimekusibu hadi uje kusema kwamba huu ulikuwa ni usanii?

Steve Nyerere: Sijatishwa na yoyote. Nlifanya vile kumlidhisha Mama, nlikuwa sina jinsi. Kuna kesi za kutishwa, kesi za kuhijiwa sio za kutishwa, sasa nitishwe na nani?

Swali: Kundi la Mama ongea na Mwanao hawajajitokeza kumtembelea Wema, Nini kinaendelea? Nini unamwambia Wema?

Steve Nyerere: Kumuona mtu ni utashi wa Mtu. Inategemeana na dada alikuwa anaishije na Wasanii wenzake, na inategemeana na hii kesi ilikwa ianhusu kitu gani. Hii kesi ni maelezo tu. unaendeleaje? Unaweza kwenda pale polisi ukakamwata..eheee tulikuwa tumekusahau, bora umekuja.

Steve Nyerere: Nlikuwa nafanya kitu Wema asipotee, Kapote.

Steve Nyerere: Maisha ni popote, mimi maisha yangu ni CCM, yeye maisha yake ameona ayaendeleze kule. CCM ni kama maji, unaweza kuchota weee. Chama cha Mapinduzi (CCM) ni kama bahari, unachota maji lakini bado ipo, wametoka wangapi”

Swali: Wewe na wema mnaukaribu je alipewa chochote?

Steve Nyerere: Hilo halinihusu

Swali: Uliongea na Mama wema kumlidhisha kwanini?

Steve Nyerere: Kwa ukaribu wa mimi na Dada yangu inabidi uoneshe support. Hata kupokea simu ni support, wengine walizima. Ningesema mama mtoto ndo anaondoka hivyo, angepata mshituko angedondoka tii shughuli imeisha. Kama ndugu nlikuwa namtia moyo.

Swali: Wewe kama Mwenyekiti wa Mama ongea na Mwanao, Kwenye kampeni za 2015, je mnaidai CCM?

Steve Nyerere: Mimi na cabinet ya Mama ongea na Mwanao na aliyekuwa makamu mwenyekiti wangu Wema Sepetu, hatuidai CCM hata senti moja, tulimalizana pale CCM Lumumba. Na matokeo yake tumempata rais bora mchapa kazi. Tafuta msanii yoyote wa mama ongea na mwanao muulize nani anaidai CCM hata senti tano

JamiiForums

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364