-->

Mboto Amuombea Msamaha Tunda Man kwa Hili

Mchekeshaji nguli wa bongo movie Mboto Haji amemuombea msamaha msanii wa bongo Fleva Tunda Man kwa kauli yake ya kudanganya mashabiki zake

Mboto

Mboto Haji

Kauli hiyo ilidai kuwa wapo kambini wakiandaa filamu itakayo kuja kwa jina la Mama Kijacho kama ilivyo wimbo wa mama kijacho ambapo video yake imemuonyesha Mboto na Riyama Ally.

Baada ya Tunda Man kuwaomba radhi mashabiki wake kwa kudanganya, eNewz haikusita kumtafuta Mboto Haji ili kufahamu kauli yake, ambapo naye alimuunga mkono Tunda Man kwa ujasiri wa kukiri kosa hadharani na kuomba msamaha.

Mboto alisema “Nawaomba mashabiki wa bongo fleva na bongo movie kumsamehe Tunda Man kwa kauli yake hiyo aliyoitamka ambayo haikuwa na ukweli ndani yake”.

Hata hivyo Mboto aliwageukia wanaoingia kwenye fani ya usambazaji wa kazi za wasanii ikiwemo filamu na kusema kuwa hawaiwezi kazi hiyo na wawaachie wajuzi wa kazi hiyo waifanye ili kukuza kipato kwa wasanii.

eatv.tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364