-->

Mtangazaji Paul James ‘PJ’ Arudi Clouds FM

Paul James ‘PJ’ amerejea tena Clouds FM akitokea EFM. Anakuwa mtangazaji wa pili wa EFM kuchukuliwa na Clouds katika kipindi cha mwezi mmoja, baada ya Kicheko.

pj

Mtangazaji PJ (mwenye kofia) akiwa na watangazaji wa kipindi cha xxl

PJ aliyeondoka Clouds mwanzoni mwa mwaka huu akiwa na Gerald Hando, ametambulishwa rasmi Jumatano hii. Anamfuata mtangazaji mwingine aliyehama Clouds akaenda EFM na kisha kurejea tena kwenye kituo hicho, Gardiner G Habash.

Mtangazaji huyo anayesifika kwa uhodari wa kuchambua magazeti, alikuwa na mchango mkubwa wa kukifanya kipindi cha Joto la Asubuhi cha EFM kujipatia umaarufu ndani ya muda mfupi. Kupokonywa kwa PJ EFM kunachocheza zaidi uhasama kati yake na Clouds FM.

 

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364