-->

Mc Pilipili Apata Ajali Nakulazwa Bugando

Mchekeshaji maarufu nchini, Emmanuel Mathias maarufu Mc Pilipili amepokewa katika kitengo cha dharura cha Hospitali ya Rufaa Bugando, Mwanza baada ya kupata ajali mkoani Shinyanga.

Ofisa uhusiano wa hospitali hiyo, Lucy Joseph amethibitisha kupokewa Mc Pilipili na amesema taarifa zaidi kuhusu hali yake zitatolewa baadaye.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Simon Haule akizungumzia ajali hiyo, amesema Mc Pilipili alikuwa akimkwepa mwendesha baiskeli katika Kijiji cha Bubiki, Kata ya Mondo mkoani humo.

Amesema mchekeshaji huyo alikuwa akiendesha gari lililopata ajali akiwa na abiria mmoja ambaye naye amepata majeraha.

Katibu Muhtasi wa Kampuni ya Pilipili Events, Stella Maswenga amesema wamepokea taarifa za ajali hiyo leo Jumanne jioni.

“Bado tunahangaika, nafikiri wamepoteza kila kitu kwa maana simu zao hazipo hewani, pia hatuna taarifa zozote kuhusu wao zaidi ya kuambiwa wamewahishwa Bugando,” amesema.

Maswenga amesema Mc Pilipili alialikwa mkoani Shinyanga kwa ajili ya kusherehesha harusi wikiendi iliyopita na alikuwa akisafiri kuelekea Mwanza.

Mwananchi

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364