-->

Mchekeshaji Mboto: Kitu ambacho hawezi kusahau kutoka kwa Aunty Ezekiel

Mchekeshaji Mboto Haji ameamua kumshukuru kwa mara ya kwanza hadharani muigizaji Aunty Ezekiel ambaye alimuonyesha upendo wakati anaugua na alipolazwa hospitalini na shukrani hizo ameziandika kupitia ukurasa wake wa instagram.

Mboto ameandika ujumbe huu kupitia ukurasa wake wa instagram “Wewe ndo jembe langu, mchiz waaaaaangu, kuna kipindi nilisumbuliwa na tatizo la moyo uliacha ratiba zako na ukawa unachoma mafuta kunifata kutoka Mwananyamala hadi jet lumo kisha ukanipeleka hospital maeneo ya Leader’s Club na kunirudisha”

“Nahis wewe umesahau ila Mimi sijasahau na kila siku najiuliza Dada yangu kipenz nikufanyie nini nilipe japo robo ya ulionifanyia nakosa na siku zinaenda.”-Mboto

“Mimi muungwana nakukumbuka sana @auntyezekiel kwa yote mema na inshaallah mwenyez mungu akufanyie wepes. Namiss kukuona nimemiss kufanya kazi tukiwa pamoja unathaman kubwa sana kwangu Dada yangu kipenz @auntyezekiel” -Mboto

Mboto amefanya kazi nyingi za kisanaa na Aunty Ezekiel zikiwemo movie kama mama Kijacho, House girl& boy, Pumba, Nampenda mke wangu na nyingine nyingi.

PROMO – NAMPENDA MKE WANGU

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364