-->

Mchuano Mkali TDFAA 2015, Jimmy Mafufu, Mike Sangu, David , Dile , Salum Chilwa

MCHUANO mkali katika kinyang’anyiro cha kugombea nafasi ya mwenyekiti wa chama cha waigizaji Taifa (TDFAA) huku wasanii wenye ushawishi kwa wasanii wenzao wakijitokeza kuchukua fomu za kugombea nafasi hiyo anasema katibu Twiza.

Jimmy Mafufu akichukua fomu ya kugombea kutoka kwa katibu wa TDFAA Twiza Mbarouk .

Jimmy Mafufu akichukua fomu ya kugombea kutoka kwa katibu wa TDFAA Twiza Mbarouk .

“Mchuano ni mkali kila mhusika amepanga kuwa ni mshindi katika kinyang’anyiro cha kugombea nafasi ya uenyekiti Kitaifa kwa chama cha Waigizaji, hadi sasa ni zaidi ya wasanii wane wameshachukua fomu za kugombea,”anasema Twiza.

Moja kati ya wasanii waliojitokeza kuchukua fomu ni pamoja na Mwenyekiti wa chama cha Waigizaji Temeke Fredy Sumari ‘Dile’, Jimmy Mafufu, Eliya Mjata ‘Davi’, Michael Sangu ‘Mike Sangu’ na Salum Chilwa huku kwa upande wa Makamu mwenyekiti akiwa ni mtu mmoja tu ambaye ni Lumole Matovulwa ‘Biggie’

FC

Comments

comments

Post Tagged with ,

Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364