-->

Mdogo wa Ndikumana Awachana Bongo Movie

Mdogo wa marehemu Hamadi Ndikumana ambaye alikuwa mume wa muigizaji wa filamu Tanzania Irene Uwoya, anayeitwa Laddy Ndikumana, amesema waigizaji wa filamu wa bongo (bongo movie ) ni wajinga, kutokana na mambo yao wanayoyafanya.

Laddy ameyasema kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, na kusema kwamba waigizaji hao ni wajinga na wanafiki kwa kuwa wameshindwa kufika kwenye msiba wa kaka yake Ndikumana, ambaye wakati wa uhai wake walijifanya kuwa rafiki yao na kumpenda.

Laddy ameendelea kwa kusema kwamba wakati marehemu Ndikumana alipokuwa na pesa, wasanii hao walikuwa marafiki na kula naye bata, lakini wameshindwa kujitokeza kwenye msiba, na kumuacha Irene Uwoya peke yake kwenda Rwanda.

Msikilize hapa chini

EATV.TV

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364