-->

Sina mpango wa kurudi CCM – Wema Sepetu

Malkia wa filamu nchini, Wema Sepetu amemwambia muigizaji mwenzake wa filamu ambaye ni kada wa CCM, Steve Nyerere kwamba hana mpango wa kurudi tena CCM.

 

Wema amesema hayo baada ya kuona ujumbe wa Steve Nyerere kumpongeza Alberto Msando kwa uamuzi wake wa kukihama chama cha ACT Wazalendo ya kwenda Chama Cha Mapinduzi, CCM.

“HAHAHAHAHAHAHAHAHAHA SASA UTAKUWA MZALENDO WA KWELI , MSANDO NAESHIMU MAAMUZI YAKO MAANA NI MAAMUZI SAHIHI, KWAKO PAMOJA NA FAMILY YAKO , RAFIKI ZAKO NASI TUPO PAMOJA NAWE, SOON NA YULEEEEEEEEE RAFIKI YETU , DADA ETU , MSANII MWENZETU , NAYE YUPO NJIANI KURUDI NYUMBANI, COMING BACK TIVU , WELCOME MSANDO,” aliandika Steve Nyerere.

Baada ya kauli hiyo, Wema Sepetu aliamua kuweka mambo sawa juu ya kauli hiyo huku akidai kwamba hana mpango wa kuhama Chadema na kurudi CCM.

“I hope hauniongelei mimi… Maana mawazo hayo sina,” aliandika Wema Sepetu.

Muigizaji huyo alikihama chama hicho baada ya kudai kuna mambo ambayo hayaendi sana ndani ya chama hicho.

Bongo5

 

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364