-->

Mdukuzi Amenirudisha Sana Nyuma- Ray C

Mkongwe wa muziki wa bongo fleva Rehema Chalamila ‘Ray C’ amedai kumfunga mwizi aliyedukua (hack) ukurasa wake wa Instagram uliokuwa na wafuasi zaidi ya laki tano na kusema kwamba hataweza kuvumilia wezi kuendelea kuwepo mitaani.

Rehema Chalamila ‘Ray C’

Ray C amefunguka hayo siku chache zilizopita alipokuwepo kwenye Heshima ya Bongo fleva kwenye kipindi cha Planet Bongo kinachorushwa kupitia East Africa radio huku akiesema, wezi hao wa mtandaoni wanarudisha wasanii nyuma katika kufanya shughuli zao.

“Mwizi aliyedukua (hack) akaunti yangu amenirudisha sana nyuma kwani nimeshindwa kufanya matangazo ya video ya wimbo wangu, matokeo yake nimetumia nguvu kubwa sana nilipouachia. Nikimkamata huyo mtu aliyenifanyia hivyo cha kwanza nitamnasa kofi kwa kunipa kazi cha pili lazima nimfikishe polisi na mwisho wake ni Segerea. Siwezi kuendelea kuvumilia watuibie halafu waendelee kukaa mitaani kwani watatutesa sana,” Ray C.

Pamoja na hayo Ray C ameongeza kwamba “Mimi akaunti yangu haijapotea kabisa kwani naiona ikiweka matangazo mbalimbali yaani nikimkamata sitamwambia anipe asilimia kumi bali atatoa pesa yote kwani nitahesababu tangazo la kwanza mpaka la mwisho ili kujua ni kiasi gani cha pesa anatakiwa anipe maana wameshazoea,” aliongeza

EATV.TV

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364