Kesi ya Wema Sepetu Yaanza Kuunguruma Mahakamani
Kesi ya matumizi ya madawa ya kulevya inayomkabili malkia wa filamu nchini Wema Sepetu na wenzake wengine wawili imeendelea tena mchana wa leo katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam baada ya kuahirishwa mapema leo asubuhi.
Katika kesi hiyo imeonekana kuanza kuwavutia watu kutokana na ushindani wa vifungu vya sheria kutoka kwa mawakili wa upande wa washtaki na ule wa washtakiwa.
Mahakama imeanza kusikiliza ushahidi wa kwanza kutoka kwa upande wa Jamuhuri ambao ndio wamemshtaki mrembo huyo pamoja na wenzake hao ambao wanasimamiwa na mawakili watatu akiwemo Peter Kibatala, Jeremiah Mtobesya na Hekima Mwasigwa.
Katika upande wa Jamuhuri kesi hiyo inasimamiwa na Wakili Constantino Kakulaki. Kwa upande wa shahidi ambaye amesikilizwa leo mahakamani hapo, Elias Muhima ambaye ni Msimamizi wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, amesema February 6 ya mwkaa huu alipokea vielelezo kutoka jeshi la polisi ambapo bahasha moja ilikuwa na msokoto mmoja na vipande viwili ndani yake vikiwa na majaniaina ya Bangi kwa ajili ya kuvifanyia uchunguzi kama vinahusiana na madawa ya kulevya.
Shahidi huyo amesema alipiama uzito bahasha hiyo iliyokuwa na vielelezo hivyo na kupata uzito wa gram 1.08 na akaanza kufanyia uchunguzi wake wa awali kwa kutumia kemikali ambapo ilibadiringa rangi na kuwa ya Zambarau ikionyesha kuwa vielelezo hivyo ni aina ya Bangi.
Elias ameendelea kwa kusema kuwa katika kufanya uchunguzi wake wa pili alitumia mtambo wa HPDC katika kuvipima vipisi viwili vilivyokuwepo katika bahasha hiyo na matokeo yaliyopatikana yalionyesha kuwa vitu hivyo ni madawa aina ya Bangi.
Akiendelea kutoa ushahidi huo, Elias ameendelea kwa kusema February 8 ya mwaka huu pia alipokea sampuli ya haja ndogo kutoka kwa mtuhumiwa huyo namaba moja kwa ajili ya kuufanyia uchunguzi kwa kutumia mtambo wa HPLC na iligundulika kuwa ndani yake kuna chembe chembe za madawa ya kulevya aina ya Bangi.
Hata hivyo upande wa washtakiwa kupitia kwa Wakili wake namba moja Kibatala wameukataa ushahidi huo kutokana na kutofuata taratibu maalumu za kisheria pamoja na kukosekana kwa baadhi ya viambatanishi muhimu ambavyo Mahakama hiyo kupitia kwa Wakili wake Thomas Simba imeutaka upande wa washtaki kuvifikisha mahakamani hapo maa moja.
Kesi hiyo imeahirishwa na inatarajiwa kusikilizwa tena Ijumaa hii ya August 4 majira ya saa nne asubuhi .
Bongo5