Waziri Dkt. Mwakyembe Kukutana na Wadau wa Filamu Dar
WAZIRI mwenye dhamana ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (MB) anatarajia kukutana na wadau wa tasnia ya filamu (Shirikisho la filamu Tanzania na vyama vyake) tarehe 4 August, 2017 siku ya ijumaa kuanzia muda wa saa 2:30 asubuhi hadi 7:00 mchana katika ukumbi wa kimataifa wa Mwalim Nyerere posta.
Mhe. Waziri makundi ambayo atakutana nayo ni pamoja na Watayarishaji, Waongozaji, Waigizaji, Wasambazaji, waandishi wa miswada, wapiga picha, Wahariri, Watafutaji wa mandhari, Wachekeshaji na Walimu wa vikundi vya kuigiza.
Bodi ya Filamu kwa kutambukua kuwa filamu ni sekta muhimu sana na inahitaji kuendelezwa kulingana na hali ya ukuaji wa teknolojia inasema kuwa ‘FILAMU NI UCHUMI, FILAMU NI AJIRA, FILAMU KWA MAENDELEO ENDELEVU’ Hivyo wadau mnaombwa kufika na kujadili tasnia ya filamu kwa maslahi mapana.