-->

Meneja Amtetea Aslay kwa WCB

Meneja wa Aslay, Chambuso amemtetea msanii wake huyo kuwa hajawahi kuwa na ukaribu na Alikiba. Hilo limekuja baada ya kusambaa maneno kuwa hitmaker huyo wa ‘Muhudumu’ ameingia kwenye mgogoro na WCB kutokana na ukaribu wake na Alikiba.

Aslay

Akiongea Ijumaa hii katika kipindi cha FNL, Chambuso amesema, Aslay hajawahi kuwa karibu na Kiba na wala hakuwa na wimbo wowote ambao tayari wameurekodi kama inavyosemwa na baadhi ya watu. Ameongeza kuwa wala hakuna tatizo lolote kati ya Aslay na WCB.

Chambuso amepigilia msumari kwa kusema, nyimbo alizoachia Aslay ni kama zawadi hajaanza kufanya kazi rasmi ila baada ya kupita mwezi mtukufu wa Ramadhan wataanza kuachia nyimbo za msanii huyo rasmi.

Bongo5

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364