Mlela Anavyozidi Kuingiza Mkwanja Nje ya Bongo
BAADA ya mwaka jana kula shavu la kucheza tamthiliya nchini Kenya kwa mwaka mmoja ambalo limeisha mwezi huu, staa wa filamu Bongo, Yusuf Mlela amejikuta akichekelea baada ya kupata kazi nyingine tena.
Akipiga stori na Risasi Jumamosi, Mlela alisema ana furaha kubwa kupata kazi nyingine inayokwenda kwa jina la Nyota ambayo ni ya miezi saba wataifanya na wasanii wa Kenya pamoja na wa Tanzania ambao ni Daud Michael ‘Duma’, Salama Salmini ‘Sandra’ na Hasheem Kambi.
“Nimefurahi sana kwa kweli maana kazi ya kwanza ndiyo nimemaliza mwezi huu sasa nimepata nyingine ambayo tutaifanya kwa miezi saba, najiona mwenye bahati sana kwa kweli maana Kenya ninajifunza mambo mengi yanayohusiana na filamu, lakini pia nitatengeneza pesa zaidi kupitia kazi yangu hii,” alisema Mlela.
Chanzo:GPL