Menina La Diva Ajifungua Mtoto wa Kiume
MSANII wa Bongo Fleva aliyewahi kushiriki shindano la kusaka vipaji maarufu la Bongo Star Search (BSS), Menina, amejifungua mtoto wa kiume Februari 9 wiki iliyopita na jina la mtoto huyo bado halijafahamika.
Aidha Menina aliyewahi kutamba na wimbo wake wa ‘Dream Tonight’ alitoa taarifa hiyo kupitia mtandao wake wa Instagram ambapo mastaa wenzake wakaendela kwa kumpa pongezi kwa kujifungua salama.