-->

Mimi Mpinzani Halisi Wa Gabo Katika ‘Game’- Faita

MWIGIZAJI chipukizi anayetamba na filamu ya Ngoma ya Roho na tamthilia ya Buriani Angel Maige Alex Mgeta ‘Faita’ ametamba kuwa kwa sasa yeye anamini kuwa ndiye mpinzani wa kweli wa mwigizaji bora katika tasnia ya filamu Salim Ahmed ‘Gabo’ kwani ana uwezo mkubwa wa kuvaa uhusika na kubadilika kwa kila sinema.

Faita aka Ngosha the Don

“Unajua uigizaji ni mbinu kwani wote tunaigiza lakini lazima atokee anayefanya vizuri kuliko wengine na ndio kinachofanyika kwangu kwa sasa mimi ndio mpinzani halisi wa Gabo Zigamba najua mbinu zake na mimi nipo katika mikono iliyomtoa,”alisema Faita.

Faita ni zao la mtayarishaji mahiri katika tasnia ya filamu Bongo Jacob Stephen ‘JB’ ambaye ndio aliyemtoa msanii kama Shamsa Ford pia amewahi kufanya kazi na Gabo kupitia sinema ya Bado natafuta, JB akiongea na mwandishi wetu alisema kuwa Faita aka Gosha ni mwigizaji wa kizazi hiki na anakiri ni msanii makini anaweza kufika mbali.

“Mtu anayejiamini utamani kupambanishwa na King hata kama maandiko mfalme Daudi alipigana na Goriati kwa ushindi bila woga name napenda kupambana na washindi si dhaifu,”

Gabo

Faita ni kijana mwenye uwezo mkubwa sana katika sanaa kwani zaidi ya uigizaji lakini pia ni mahiri katika uchezaji wa ngoma za asili sarakasi na michezo mingine ambayo inamfanya awe tofauti na waigizaji wengine.

Filamu Central

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364