-->

Niva Atoboa Ukweli wa ‘Bifu’ Lake na Nay wa Mitego

Msanii wa bongo movie Niva amesema madongo yote waliyokuwa wanatupiana na Nay wa Mitego kwa mwaka 2016 ilikuwa ni ‘bifu’ za kimuziki na mipango ya kibiashara kwa upande wa movie lakini hawana bifu lolote kati yao.

Akiongea kupitia eNewz Niva amesema hawajawahi kugombana na wala hawana tatizo lolote na Nay kwa kuwa ni watu ambao wamekuwa sehemu moja wamesoma shule moja na wamekuwa wakisaidiana kwenye mambo mbalimbali hata wakati Niva anafunga ndoa Nay alimsaidia kwa kiasi kukubwa.

Hata hivyo Niva ameweka wazi kuwa mambo hayo ya kudanganya mashabiki zao wameyaacha mwaka 2016 na mwaka huu hawatakuwa na mambo kama hayo kwa kuwa ni mwaka wa mafanikio zaidi kisanaa.

eatv.tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364