Mimi Nina Majumba sio Nyumba-Steve Nyerere
Msanii mkongwe wa filamu Steve Nyerere amedai yeye ni mmoja kati ya wasanii ambao wanamiliki nyumba nyingi lakini hataki kuzionyesha.
Akiongea katika kipindi cha Uhondo cha EFM Jumatano hii, Steve Nyerere amedai yeye haoni ufahari wa kuonyesha mali alizonazo kama wanavyofanya baadhi baadhi ya wasanii.
“Mimi nina majumba sio nyumba ila sitaki kuonyesha instagram,” alisema Steve Nyerere. “Pia kuna nyumba kubwa ambayo ndiyo nitaamia ikiisha, kwa sasa hivi nimepanga Mkwajuni Kinondoni na naishi na familia yangu,”
Katika hatua nyingine mwigizaji huyo amewataka watanzania kuhudhuria show yake ya ‘East African STANDUP COMEDY’ ambayo itafanyika kwa mara ya kwanza Jumamosi katika hotel ya Protea jijini Dar es salaam.
Bongo5