Mke wa Chameleon Adai Talaka Mahakamani
MKALI wa muziki nchini Uganda, Jose Chameleon na mke wake, Daniella Atim, wanaweza kuachana hivi karibuni baada ya mwanamke huyo kwenda mahakamani kwa lengo la kudai talaka.
Wawili hao walifunga ndoa Aprili 18, 2017 na wana watoto wanne ila kwa sasa wanaweza kuachana, huku mrembo huyo akidai kuwa ananyanyaswa mno na Chameleon.
Kwa mujibu wa Daniella, miezi ya hivi karibuni amekuwa akitishiwa maisha na amekuwa akikosa uhuru ndani ya ndoa hiyo.
“Nimekuwa nikiteseka kwenye ndoa yangu kwa sasa, sina furaha kabisa kwa kipindi cha miezi ya hivi karibuni, hivyo nadhani huu ni wakati wangu wa kufanya maamuzi sahihi ili niwe huru, nifurahie maisha yangu, nahitaji talaka na tayari nimepeleka taarifa mahakamani,” alisema Daniella.