-->

MO Music Atoboa Siri ya Kutengana na Baraka

Nyota wa Bongo Fleva kutoka jijini Mwanza MO Music amefichua sababu ya kundi la Wazawa, na kueleza kuwa ugomvi binafsi wa T Nocks na Baraka The Price ndiyo uliopelekea kundi hilo kuvunjika.

mo23

Mo Music alikuwa ni memba wa kundi hilo lililokuwa likiundwa na wasanii kutoka lililojulikana kwa jina la WAZAWA, lililokuwa likiundwa na yeye (MO Music), Baraka The Prince pamoja na T Nocks.

Mo aliongeza kuwa “Kila mtu ana akili zake tofauti na utofauti huo ndiyo uliopelekea Wazawa kushindwa kudumu, mara nyingine miongoni mwetu wengine walikuwa wanajiona bora zaidi ya wengine”.

Pia Mo Music aligusia kwa kusema sababu ya ugomvi wa Baraka na T Nocks kuwa ni wimbo wa So Fly, wimbo ambao ulimtambulisha Baraka vizuri hasa kwa mkoa wa Mwanza.

eatv.tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364