-->

Nipo Bongo Kumfuata Jack Wolper- Burundiano

THAMANI ya Lugha yetu ya Kiswahili katika filamu kwa nje ni kubwa sana hadi wasanii wakubwa wameingia darasani kwa ajili ya kuigiza kama watanzania msanii mkubwa nchini Burundi Sururu Jafari ‘Burundiano’ nafunguka na kujivunia kuijua lugha hiyo na yupo nchini Tanzania akirekodi filamu na wasanii wa Bongo.

Sururu jafari

Burundiano akikagua vifaa vya Production kabla ya kuanza kazi Tanzania

Sururu Jafari

Burundiano akiwa katika pozi la picha.

Hemed suleiman, Sururu Jafari, Wise mulmul

Burundiano akiwa katika kikao na Director Wise Mulmul, Hemed Phd.

Jack Wolper, Sururu Jafari, Wise

Burundiano akiwa katika kikao na Jack Wolper

“Lengo langu ilikuwa kuwa mwigizaji mkubwa wa kimataifa lakini wakati huo nilikuwa najua lugha ya Kifaransa tu, nikaona fursa katika filamu za Kitanzania nikajifunza Kiswahili na ninafanya kazi na ndugu zangu Watanzania,”alisema Burundiano.

“Nimekuja hapa kumfuata Jack Wolper na kufanya naye kazi kubwa kabisa hapa na nchini Burundi inshort stars wa Tanzania watashirikiana na wasanii kutoka nchini kwetu ni kazi nzuri sana ambayo itapendwa sana,”

Msanii huyo maarufu nchini Burundi na Rwanda yupo nchini akiandaa filamu mpya aliyoipa jina la Burundiano In Dar sinema inayowashirikisha Jack Wolper, Hemed Suleiman ‘Phd’ na inaanza kurekodiwa Dar Es salaam na kumaliziwa nchini Burundi katika mji wa Bujumbura, amefanya hivyo akiamini kuwa huku ndio soko kuu.

Mwigizaji huyo nyota yupo nchini na muongozaji wa filamu mahiri kutoka Burundi Wise ambaye amejizolea umaarufu nchini humo na Rwanda kwa kazi zake nzuri Wise tayari amefanya kazi moja kubwa na kuwashirikisha wasanii kutoka nchini Tanzania akimshirikisha Shamsa Ford sinema hiyo inaitwa Najuta Shamsa.

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364