Shilole na Nuh Mziwanda Wamaliza Nifu Lao
Ilikuwa ni ‘break up’ iliyofuatiwa na uadui mkubwa. Ilipelekea hadi Nuh Mziwanda kuandika wimbo ‘Jike Shupa’ uliomlenga ex wake Shilole.
Haikuishia hapo, wawili hao waliendelea kurushiana maneno kwenye mitandao ya kijamii na kwenye mahojiano na kulaumiana kwa mengi. Hata hivyo mlalamikaji mkubwa alikuwa Nuh aliyemwelezea Shishi kama mwanamke aliyempotezea muda wake na kumkwamisha kwenye muziki.
Pia wimbo wa Shilole, Say My Name una mashairi yanayotaka kuhusiana na vunjiko la huba kati ya mastaa hao waliotengeneza vichwa vya habari wakiwa pamoja ikiwa ni pamoja na kujichora tattoo za majina yao.
Na sasa huenda wameamua kuyaacha yaliyopita yapite na wagange yajayo. Alhamis hii wawili hao waliweka picha zao kwenye Instagram kwa mara ya kwanza tangu waachane.
Akiweka picha ya Nuh kwenye akaunti yake ya Instagram, Shilole aliandika: God Bless You.