Mpira Dakika 90 Unachosha- Wema Sepetu
Mrembo na staa wa filamu za Kitanzania, Wema Sepetu, amefunguka kuwa mchezo wa soka unamchosha kuangalia kwa kuwa unatumia muda mrefu wa dakika 90 huku wachezaji wake wakihangaika mno kutafuta bao tofauti na mpira wa kikapu.
Wema Sepetu, alilidokeza Swaggaz, kuwa mara nyingi akiwa nyumbani kwake huwa anaangalia mpira wa kikapu kwani hauchoshi na wachezaji huwa wanatumia muda mfupi kupachia mabao.
“Mpira wa miguu unanichosha, siwezi kuvumilia dakika 90 zote ziishe kwani ni muda mrefu tofauti na ilivyo kwenye Basketball, ambapo mabao yake hupatikana kirahisi na mchezo hauchukui muda mrefu,” alisema Wema Sepetu.
Aliongeza kuwa ili aangalie soka na kumaliza muda wote wa mchezo ni lazima awe na kampani yake na mara nyingi iwe laivu uwanjani.
Mtanzania
NUNUA FILAMU KUTOKA STEPS ENTERTAINMENT: TUNAKUFIKISHIA POPOTE PALE ULIPO:
Piga namba hizi: 0673 348 364 au 0754 256 489.
KAMA WEWE NI MFANYA BIASHARA UNATAKA KUWA WAKALA WA KUSAMBAZA FILAMU POPOTE PALE:
Piga namba hizi: 0673 348 364 au 0754 256 489.
Filamu Zilizotoka Hivi Sasa >>>>HIZI HAPA