Sitoacha Kuigiza Sababu ya Gospel – Senator Msungu
MWIGIZAJI wa filamu kutoka Swahilihood Stanley Msungu ‘Senator Msungu’ amefunguka kwa kusema kuwa kufuatia yeye kuimba na kuokoka hawezi kuacha uigizaji bali kila jambo atalipa nafasi yake kwa wakati.
“Nafanya Gospel kama sehemu ya aina yake ya uhubiri, nimetoa wimbo unaitwa Nimerudi na nitaendelea na uigizaji pia kwani ni vipawa vyote kutoka kwa Mungu,”anasema Msungu.
Msungu anasema kuwa yeye anajitofautisha na wasanii wengine wa filamu ambao baada ya kufanikiwa katika muziki upumzika kuigiza lakini yeye ataendelea kuigiza pamoja na wimbo wake wa Nimerudi kufanya vizuri kwa vyombo Runinga na Redio za kidini bado anaigiza.
SENETA anaigiza katika tamthilia mbalimbali kwa hivi sasa anafanya vizuri katika tamtilia ya Usaliti akiwa na waigizaji nguli kama Nyamayao, Chuchu Hans, Thea na wasanii wengineo na uruka East Africa Tv.
FC