-->

Msanii Engine Atoboa Siri ya Kumchukua Wolper

Msanii wa muziki wa kizazi kipya Engine ambaye hivi karibuni kulikuwa na tetesi za kumng’oa Jackline Wolper na kumuweka ndani, ameweka wazi sababu za kuamua kumtumia msanii huyo kwenye kazi yake.

Akizungumza kwenye Friday Night Live Engine amesema Wolper ni miongoni mwa wanawake wachache Tanzania wanaojitambua, na ndio sababu iliyomfanya asifikirie mara mbili kumfuata.

“Wolper ni mwanamke jasiri, mwanamke anayejitambua , anajituma yuko fit kila idara, na ndio maana nikamfuata”, amesema Engine.

Msanii huyo ambaye ameachia kazi yake mpya, amewaomba watanzania kufuatilia kazi zake kwani alishafanya kazi nyingi siku za nyuma lakini hazikuwahi kufanya vizuri.

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364