-->

Nicole Aingilia Ishu ya Wastara Kuchangiwa Pesa

MSANII wa filamu Bongo, Nicole Francklyn amewataka wasanii wenzake kuungana na kuendesha kampeni ya kumchangia msanii mwenzao, Wastara Juma kutokana na maradhi ya mguu yanayomsibu, kwa kuwa hakuna aijuaye kesho.

Nicole Francklyn

Akizungumza na Star Mix, Nicole alisema, kama wasanii wangekuwa na umoja na kuungana katika hilo, kwa jinsi ambavyo wamekuwa wakijionyesha kumwaga pesa kwenye mambo ya starehe, endapo wangejitoa kwa moyo mmoja kwenye suala hilo, basi kivyovyote vile michango ingekuwa imetimia.

“Niwasihi wasanii wenzangu tuungane kumchangia Wastara michango iweze kutimia akamilishe matibabu yake, naamini sapoti ya wasanii iliyopo bado haitoshi waongeze nguvu kwenye hili, hata kama mtu ana visasi naye aweke kando kwa sasa, kwa sababu matatizo yanaweza kumfika yeyote yule,” alisema.

Chanzo:GPL

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364