Msimu Mpya wa Siri za Familia Umerejea Kwa Kasi
ILE Tamthilia maarufu inayotamba kwa sasa ya Siri za Familia ambayo urushwa na kituo cha Televisheni cha East Africa Television (EATV) imekuja sehemu ya pili kwa msimu mpya huku ikitabiriwa kuteka zaidi wapenzi wa tamthilia Swahilihood baada ya kufanya vizuri katika msimu uliopita.
Akiongea na FC mtunzi wa Siri za Familia Said Mkukila ameiambia FC kuwa msimu mpya wa Siri za Familia ni burudani ya aina yake kutokea Bongo hivyo wapenzi wa tamthilia waipokee kwa nguvu zote kwani ni kazi ya kisasa kabisa na iliyolenga kufundisha na kuiburudisha jamii.
“Tumejipanga kwa kila idara Siri za Familia msimu mpya ni moto wa kuotea mbali, kuanzia uandishi wa script uchezaji na hadithi yenye kwa ujumla wake vimeandaliwa vizuri sana ni kila irukapo usikose mpenzi wa vitu vizuri,”alisema Mkukila.
Siri za Familia itakuwa ikiruka kila siku ya Jumatatu, Jumanne, Jumatano na Alhamisi kuanzia saa 12:30 jioni kupitia Televisheni ya Eatv tamthilia hiyo inaandaliwa na kampuni ya Jasons. Si ya kuikosa ni Burudani kwa wanafamilia.
Filamu Central