-->

Mtitu Awachana Viongozi wa Shirikisho la Filamu Tanzania

DAIREKTA mwenye jina kubwa nchini, William Mtitu amefunguka kuwa kitu kinachoiangusha tasnia ya filamu Bongo ni uongozi wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF), ambao umeshindwa kuwasimamia wasanii wake vizuri pamoja na kutengeneza mazingira mazuri ya kuwafanya wadau mbalimbali kuvutiwa na tasnia hiyo hata kuwekeza.

mtitu

Akichonga na gazeti hili, Mtitu aliongeza kuwa ili tasnia ya filamu iweze kusimama na kusonga mbele au angalau tu kurudi mahala ilipokuwa siku za nyuma ni lazima uongozi wa TAFF uwe thabiti ikiwezekana yafanyike mabadiliko makubwa katika uongozi huo na wapatikane viongozi wazuri wa kuwasimamia wasanii katika ukuzaji wa tasnia ya filamu.

“Unapoona kundi lenye viongozi linashindwa ni dhahiri kuwa viongozi wake si thabiti. Ndivyo ilivyo kwenye filamu, hii sintofahamu inayoendelea iliyoshusha tasnia yetu ni ukweli kuwa huwezi kuwalaumu tu wasanii, viongozi wa TAFF wanahusika kwa namna moja au nyingine,” alisema Mtitu.

Chanzo:GPL

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364