Mtoto wa Mwigizaji Ray na Chuchu Hans Apata Ubalozi wa NMB
MTOTO wa Staa wa Filamu Bongo, Vicent Kigosi ‘Ray’, aitwaye Jaden Kigosi, amepata shavu kutoka kwa wazazi wake baada ya kumfungulia akaunti ya ‘NMB Mtoto Akaunti’ kwa ajili ya akiba itakayoweza kumsaidia hapo baadaye.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kumfungulia akaunti hiyo, Makao Makuu ya Benki ya NMB, Posta jijini Dar, Ray alisema kuwa, huo ni uamuzi aliouchukua yeye na mwenzi wake Bi Hans baada ya kuridhishwa na huduma za Benki ya hiyo. Pia kutokana na kushawishika na umahiri wa umahususi wa akaunti hizi za mpango wa NMB Mtoto Akaunti.
“Niwaombe tu mastaa wenzangu kuwa, suala la mtoto kumfungulia akaunti benki ni muhimu sana kwani sisi wazazi tupo leo lakini hatujui kesho yetu itakuwaje?
“Ili usimnyime haki ya maisha mazuri mwanao hapo baadaye, basi ni jukumu la kila mmoja kuhakikisha anamfungulia akaunti mwanaye ila hata asipokuwepo ataweza kusoma bila shida,” alisema Ray.
Ray aliambatana na mzazi mwenzake ambaye pia ni msaniiwa Bongo Movies, Chuchu Hans katika kumfungulia mtoto wao NMB Mtoto Akaunti.
Kwa upande wake Meneja Huduma za Kibenki NMB, Caroline Mosha, ametoa wito kwa walezi na wazazi kuwa na utamaduni wa kuwafungulia akaunti watoto na vijana wao bila kusahau kuwahimiza kuhusu elimu ya fedha#NMBWajibu. www.nmbbank.co.tz/wajibu