-->

Muonekano Mpya wa Nywele za Kijani za Ben Pol Zampa Dili Nono

Wakati wabongo wakiendelea kumshambulia mitandaoni kwa aina ya mtindo wa kupaka rangi za kijani kwenye nywele zake, Msanii Ben Pol ameneemeka na staili hiyo kwani ameshalamba dili nono na kampuni ya Green Telecom inayojihusisha na masuala ya mawasiliano na IT.

Ben Pol amethibitisha taarifa hizo kwenye mahojiano yake na Bongo5 ambapo amesema ni kweli amepata dili hilo na tayari ameshasaini mkataba lakini maelezo mengine atayatoa baadae baada ya kumaliza baadhi ya vitu na kampuni hiyo.

“Ni kweli nimepata dili nzuri yenye mkataba kabisa na Green Telecom lakini kwa sasa bado kuna vitu vinamalizika halafu tutatoa taarifa kamili na wenyewe ila ni dili kubwa,“amesema Ben Pol.

Huu ni muendelezo wa mafanikio kwa Ben Pol kwani mwishoni mwa mwaka jana alipata dili kadhaa ikiwemo ya ubalozi wa MAÜA association.

Comments

comments

Post Tagged with

Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364