Muziki Wangu ni Zaidi ya ‘Kiki’ – Belle 9
Nyota wa Bongo fleva nchini, Belle 9, ambaye kwa sasa katia kambi Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuusimamisha vyema muziki wake, amesema kuwa anaamini kazi yake ni kubwa zaidi ya kiki zilizozoeleka kutafutwa na wasanii.
Belle 9 amezungumza hayo na eNewz ambapo amesema muziki wake una nguvu tofauti na kiki ambazo zimezoeleka hapa mjini kutoka kwa wasanii mbalimbali wanavyo tumia mapenzi, skendo, familia n.k ili wajulikane au wazungumziwe.
“Muziki wangu ni mkubwa kuliko kiki ambazo zinaendelea hapa mjini kwa mfano kuonesha familia yangu, kwa kuwa yale ni maisha yangu binafsi na familia yangu ambayo haipo tayari kujulikana pia” aliongeza.
Belle 9 amesema kuwa kama mtu anataka kutafuta ‘kiki’ kuhusu yeye, Basi itamlazimu aishi karibu naye sana au na familia yake ili kutengeneza ‘kiki’ japokuwa bado itakuwa ni ngumu kutokana na mfumo wa maisha anaoishi kwa kuwa hapendi kuzungumziwa mbali na muziki.