-->

Mwakifamba, Kipemba Kugombea Urais

KAMATI ya Uchaguzi wa viongozi wa Shirikisho la Filamu nchini (TAFF), imetangaza majina ya watakaogombea katika uchaguzi utakaofanyika katika Ukumbi wa Urafiki, Ubungo, Februari 20 mwaka huu.

kipemba-na-mwakifamba

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa kamati hiyo, Mathew Bicco, alisema uchaguzi huo utakuwa na nafasi tatu za kugombania ambazo ni urais, makamu wake na ujumbe wa bodi.

“Katika nafasi ya Rais wagombea ni Simon Mwakifamba na Issa Kipemba, nafasi ya Makamu wa Rais ni Deosonga Njelekela na nafasi ya ujumbe wa bodi ni Ummy Mpallu, John Kallaghe, Daniel Rugaibura, Irene Sanga, Mwanaharusi Mela, Ally Dad, Hussein Kimu, William Mtitu, Single Mtambalike, Michael Sangu, Juma Chikoka, Adamu Jumal na Abdulazizi Babuu,” alieleza Bicco.

Bicco alisema uchaguzi huo utaanza saa 4:00 asubuhi na ratiba ya mkutano mkuu wa Shirikisho hilo utakuwa ni moja ya agenda kuu.

Mtanzania

Comments

comments

Post Tagged with

Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364