-->

Mwana FA Akiri ‘Kutia Chumvi’ Kwenye Dume Suruali

Mkongwe wa Rap ndani ya Bongo, Mwana FA, amesema siyo kila kitu alichoimba kwenye ngoma yake inayotikisa hivi sasa ya ‘Dume Suruali kina uhalisia, huku akikiri ‘kutia chumvi’ nyingi kwenye wimbo huo.

FA amefunguka hayo alipokuwa kwenye show kubwa ya kila Ijumaa saa 3;00 ya FNL inayoruka kupitia EATV, na kuwatoa hofu mashabiki wake hususani mabinti kutoogopa maneno yaliyotumiwa kwenye wimbo huo kwa kuwa mengi aliyatumia ili kunogesha wimbo wake.

“Kweli nimetia chumvi nyingi kwenye Dume Suruali, na imani yangu mimi hakuna negative publicity kwenye muziki na contraversy ndizo zinazouza, kwahiyo nisingeweza kuongea ukweli tu mwanzo mwisho, ili kutia chumvi kidogo ili ngoma iwe gumzo, ingawa nimeimba vitu vya ukweli, lakini si vyote vyenye uhalisia” Amesema Mwana FA

Baadhi ya mabinti wamekuwa wakilalamikia kusingiziwa mambo kadhaa yaliyoimbwa katika wimbo na kudai kuwa hakuna wasichana wenye tabia hizo, jambo ambalo Mwana FA amelazimika kutoa ufafanuzi na kuongeza kuwa mara nyingi ngoma anazotoa ni lazima ziwe na utata na kuzua mijadala.

Pamoja na hayo Mwana FA amesisitiza kuwa maudhui ya wimbo huo kiujumla ni kutoa somo kwa wasichana wa aina hiyo wenye tabia ya kuingia kwenye mahusiano kwa lengo la kutafuta kipato.

Aidha ameweka wazi ujio wa ‘collabo’ yake na wakongwe wenzake Fid Q na AY, ambayo amesema iko tayari na muda wowote itakuwa hewani.

eatv.tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364