-->

Shilole Ndiye Aliyenitongoza – Hamadai

Msanii wa bongo fleva Hamadai ambaye  aliwahi kuwa mpenzi wa msanii mwenzake Shilole amezungumza na eNewz na kutokwa na povu kuwa, Shilole ndiye aliyeanza kujipendekeza kwake na kumsumbua kwa muda mrefu akitaka wawe wapenzi.

Hamadai ni msanii mchanga wa bongo fleva ambaye watu wengi walimfahamu mara baada ya kuwa katika mahusioano na Shilole.

Amesema kuwa kwa sasa ameamua kuachana kabisa na Shilole kwa sababu kuna mambo ambayo alikuwa akiona hayaendi sawa na sasa ameamua kujikita katika muziki wake.

“Shilole ndiye aliyenitongoza mimi na siyo mimi, na sasa nimeona niachane naye kwa sababu kuna vitu ambavyo nilikuwa naona haviendi sawa, pia mimi siwezi mzungumzia vibaya. Kabla yangu alikuwa na watu kadhaa ambao tayari ameachana nao, akawa na mimi na tukaachana na sasa ana mtu mwingine ambaye pia  anaweza kuachana naye, hayo ni maisha yake na mimi siwezi kumuingilia” Alisema Hamadai.

Pia aliongezea kuwa yeye sasa hivi amejikita sana katika muziki na kuachana  na Shilole hakujampunguzia chochote katika maisha yake.

eatv.tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364