-->

Mwanaheri Awatahadharisha Wabunge Wanaomsumbua Mitandaoni

STAA wa filamu za Kibongo, Mwanaheri Ahmed amesema kuwa anawatahadharisha wabunge wanaomsumbua mitandaoni na kwenye simu yake kuwa wakiendelea atawataja kwani anawaheshimu sana.

Mwanaheri Ahmed

Akizungumza na Risasi Jumamosi, Mwanaheri alisema kuwa kutokana na shepu aliyonayo amekuwa akisumbuliwa na wabunge tofauti kupitia akaunti yake ya Instagram ambapo humfuata DM na kwenye simu yake kumuomba kuingia naye kwenye uhusiano kitendo ambacho kinamhatarishia uhusiano wake na mpenzi aliyenaye sasa.

“Unajua nashindwa kuwataja wabunge wanaonisumbua kwasababu nawaheshimu lakini nimesema iwapo wataendelea nitawataja kwa sababu inakuwa kero na imewahi kuniharibia kwa mpenzi wangu mpaka kufi kia hatua ya kuniambia niondoke huko wakati huko ndiyo nafanya kazi zangu za biashara pamoja na fi lamu kwa ujumla,” alisema Mwanaheri.

Chanzo:GPL

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364