Unauza Filamu Elfu 6 kwa Hali Gani ya Maisha-Steve
Mchekeshaji Steve Nyerere ameendelea kufunguka mambo mengine mapya kwa kudai kinachosababisha kufa kwa filamu za bongo ni wasanii wenyewe kushindwa kutambua ushidani wa kibiashara katika soko ukoje.
Steve amebainisha hayo kupitia kipindi cha eNewz huku akisema adhani kama wanapaswa kuendelea kushindana na wamachinga wanaosambaza na kuuza ‘CD’ katika soko la Karikakoo kwa kuwa wao wanachokiuza ni kile ambacho kinauzika kwa jamii nasiyo vinginevyo.
“Sidhani kosa letu ni hawa wamachinga, machinga wanauza ‘Product’ ambayo inauzika nje. Filamu moja ya kizungu ambayo ina ‘part 1’ ni shilingi elfu mbili na mia tano (2,500), wewe ‘Part 1 &2’ unauza shilingi elfu sita (6,000) kwa hali gani ya maisha ?”. Alisema Steve
Katika hatua nyingine, Steve aliendelea kurusha lawama zake kwa wasanii kwa kudai wao ndiyo chanzo kikubwa cha kuiangamiza tasnia ya filamu kwa kuwa wengi wao hawapendi kufikilisha akili zao katika kutengeneza kazi zilizokuwa bora kwa jamii ila wanachokitazama zaidi ni kupata faida kubwa kwa kazi mbovu.
“Hiyo ndiyo sumu ambayo ipo na inatufanya mpaka leo hatupo katika umoja, kwanza ili tuweze kufanikiwa mafanikio hayapo ya mmoja mmoja, mafanikio yote duniani yalipita kwa watu ndiyo wewe ukafanikiwa kwa hiyo lazima tukubaliane, tupendane na nyoyo zetu ziwe zimefunguka kwa kufanya vitu vizuri, tunawaza sana gharama za movie kuliko kufanya kitu kizuri kwa gharama ni bora upate laki 2 faida lakini ‘site’ iseme huyu mtu ni sahihi”.Alisema Steve
Aidha Steve aliendelea kusisitiza kwamba “Kuna ma-director wazuri zaidi lakini leo wote hawapo, wanachokikosa ni ushirikiano, tunao ma-director wazuri tu, wanaweza wakafanya kitu kizuri tu ‘site’ lakini ushirikiano hawana kuna watu wanakuwa Mungu watu haiwezekani, haiwezekani kuwa Mungu mtu jamani Mungu ni mmoja tu”- Steve aliendelea kusisitiza