-->

Mwanamuziki wa Ubelgiji Atua Nchini Kufanya Kolabo na Harmorapa

Dar es Salaam. Mwanamuziki Kriticos kutoka Ubelgiji amewasili nchini kwa ajili ya kutengeneza wimbo wa pamoja na mwanamuziki Harmorapa.

Kriticos na Harmorapa

Kriticos ambaye anaimba miondoko ya kufokafoka, (rap) amesema ameupenda uimbaji wa Harmorapa na ndiyo sababu ya kuamua kufanya naye kazi.

Aliyazungumza hayo muda mfupi baada ya kutua uwanja wa ndege wa Julius Nyerere leo mchana.

Kwa upande wake Harmorapa anayetamba na wimbo wa Kiboko ya Mabishoo alisema ujio huo ni heshima kubwa kwake.

Harmorapa amewataka mashabiki wake kukaa tayari kupokea ngoma hiyo itakayotengenezwa na mtayarishaji wa muziki, P-Funk Majani.

 

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364