-->

Wauzaji wa Filamu za Nje Wapewa Siku 10 Kuacha Biashara Hiyo

WAUZAJI wa filamu za nje wamepewa siku kumi wawe wameachana na biashara hiyo kwani haifuati utaratibu kisheria na kuwaacha wasanii ambao ndio wanaofuata vigezo vya uuzaji wa filamu kuwa maskini pamoja na kufanya kazi kubwa hayo oda hiyo imetolewa na mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda.

Carlos, Dilesh, Jimmy Mafufu, Mh. Makonda, Kamanda Sirro, Odama

Akiongea mbele ya Kamanda Simon Siro na wadau wa filamu ambao ni wasanii amemwagiza afisa biashara Mkoa kuhakikisha kuwa maduka yote Kariakoo ambayo yanafanya biashara kinyume na Leseni zao zinawataka wafanye nini yafungwe mara moja bila kuchelewa huku akiwapa nafasi hiyo kwa muda huo na wakishindwa ataingia mtaani mwenyewe.

“Nimetoa muda huo ili mtafute jinis ya kuwa wasiliana na taasisi husika kam a Bodi ya Filamu, Cosota, Basata na nyinginezo katika ufanisi wa kazi hizi zisizo halali kwani wanafanya biashara wakitumia leseni hizo,”amesema Makonda

Wasanii waliokuwepo katika mkutano huo wamempongeza mkuu wa Mkoa kwa kutoa maagizo hayo kwani inawezekana ikawa ni sehemu kubwa ya wao kurudi sokoni, wasanii hao ni Vincent Kigosi ‘Ray’, Simon Mwapagata ‘Rado’, Jacob Stephen ‘JB’, Jimmy Mafufu, Jennifer Kyaka, na mkurugenzi wa Steps Entertainment Dilesh Solanki, Carlos Londwe pamoja na Moses Mwanyilu mwenyekiti wa Chama cha Wasambazaji.

kikao kikiendelea kuhusu suala Filamu

Harakati za kupambana na wauzaji wa kazi zisizo na uhalali za kutoka nje zimekuwa zikifanywa na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo mara kwa mara chini ya aliyekuwa Waziri wa wizara hiyo Mh. Nape Nnauye pamoja na Bodi ya filamu huku wauzaji hao wakikahidi kwa kufunga maduka siku chache na kurudi kwa nguvu.

Chanzo cha mauzo ya kazi hizo ni sehemu ya Kariakoo lakini mitaani biashara hiyo imetapakaa kila kona jambo ambalo linaahujumu uchumi kwani wauzaji wanatengeneza fedha nyingi bila kulipa kodi, hata hazifanyiwi ukaguzi na kuonyesha filamu zisizo na maadili.

Filamu Central

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364