-->

Mweee! Eti Senga Hajapata Mrithi

MCHEKESHAJI mkongwe katika filamu Bongo, Ulimboka Mwalulesa ‘Senga’ amesema hajapata mtu wa kuendeleza makali yake ya uchekeshaji sambamba na pacha wake Pembe bin Kichwa, licha kujaa wasanii wa kumwaga nchini.

“Filamu ni kama soka tu, zamani wachezaji wenye vipaji walikuwa wengi, ila hawakuwa na fedha, lakini siku hizi fedha nyingi lakini vipaji hakuna. Natamani sana tupate warithi wa kushika nafasi yangu na pacha wangu, Pembe lakini ndio hivyo tena,” alisema.

Mvunja mbavu huyo, ambaye amekuwa aking’ara hasa anaposhirikiana na Pembe alisema uwezo wao wa uigizaji umejengwa zaidi na ubunifu, kuzingatia muswada na kuwa na nidhamu ya kazi, kitu wasichonacho wengine kwa sasa.

Mwanaspoti

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364