Mwigizaji wa TMT Aula Rwanda
MWIGIZAJI chipukizi Shiraz Ngasa aliyeibuliwa na shindano la kusaka vipaji vya filamu kupitia Tanzania Movie Talent (TMT) amefanikiwa kuigiza filamu kubwa nchini Rwanda kama muigizaji kinara na kufanya vizuri kwa kumwagiwa sifa lukuki kulingana na kipaji alichoonyesha.
“Rwanda wamejipanga katika ujio wao wa utengenezaji filamu haikuwa rahisi kupata nafasi ya kuigiza katika filamu ya Seeds of memory kama mhusika mkuu (Steringi) nimeitanga Tanzania,”alisema Shiraz
Msanii huyo ambaye alifanikiwa kuchaguliwa baada ya usaili mkubwa kufanywa nchini Rwanda anasema kuwa amezidi kukua zaidi kwani kwa mara ya kwanza amekutana na waongozaji wa filamu kutoka Hollywood wamemjenga zaidi, sinema ya Seeds of Memory imeshirikisha nyota wa Afrika ya mashariki.