-->

Mzazi mwenzake Zari afariki dunia

Dar es Salaam. Mfanyabiashara wa Uganda, Ivan Semwanga amefariki dunia katika Hospitali ya Steve Biko Academic jijini Pretoria, nchini Afrika Kusini.

Zari aliyezaa watoto watatu na mwanamume huyo amethibitisha kifo chake kwa kuandika katika mtandao wa Instagram akimtakia pumziko la milele.

“Mungu huwaita kwake walio wema ndiyo maana amekuchukua. Umegusa maisha na kusaidia wengi. Nakumbuka ulikuwa ukiniambia maisha mafupi acha ufurahie, sasa naelewa ulichokuwa ukimaanisha… utakumbukwa daima,” anaandika Zari.

Anakumbukwa kwa staili yake ya maisha ya kuonyesha fedha katika mitandao ya kijamii na kuzigawa kwa watu wenye mahitaji mara kwa mara.

Tazama video akisaidia watu mbalimbali

 

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364