Mzee Kambi na Frank Watembelea White State House kwa Obama
WAIGIZAJI kutoka Hashim Kambi ‘Ramsey’ akiwa na msanii mwenzake Mohamed Mwikongi ‘Frank’ wamebahatika kutembelea katika viwanja vya Ikulu ya Marekani maarufu kwa jina la White State House katika jiji la Washington Amerika.
Toka New York msanii mahiri katika tasnia ya filamu Swahilihood Hashim Kambi aka Ramsey anafunguka kwa bahati hiyo ya kuweza kufika katika eneo lenye ulinzi katika kiwango cha juu pengine kuliko Ikulu nyingi Ulimwenguni, anasema amesikia faraja kubwa sana.
“Upo huku muda kidogo na tulikuja kikazi kwa maana ya kushoot filamu huku Marekani na tumemaliza salama lakini kutokana na hali ya baridi kuwa kubwa tumepuzika na tunatumia muda huu kutembelea sehemu mbambali,”ansema Ramsey.
Msanii huyo amesema kuwa akiwa na mwigizaji mwezake wameweza kufika sehemu mbambali kama sehemu ya utalii na kujifunza mambo kutoka kwa wajuzi wa filamu yaani akiaongelea Hollywood na sehemu waliyoifurahia ni kutembelea Ikulu ya Marekani New York.
FC