-->

Nitaendelea Kuwa Mwanamuziki Mpaka Nakufa-Prof Jay

Mbunge wa Jimbo la Mikumi na msanii wa bongo fleva, Joseph Haule maarufu kama Prof Jay amesema kuwa yeye ni mwanamuziki na ataendelea kufanya muziki mpaka siku atakapotoweka duniani.

prof-jay

Prof Jay amefunguka hayo baada ya Babutale kutaka kufahamu ni lini msanii huyo ataachia kazi nyingine kwani toka amekuwa mbunge wa jimbo la Mikumi amekuwa kimya kwenye sanaa na kusema kuwa amekumbuka mashairi ya msanii huyo, ndipo hapo Prof Jay alipoweka sawa kuwa kwa sasa yeye ni mbunge wa Mikumi hivyo ana kazi kubwa ya kuwatumikia wana Mikumi na kusema kwamba jambo hilo pia haliwezi kufanya ashindwe hata kwa uchache kuendelea kufanya muziki.

“Nakushukuru sana Babutale kwa kuendelea kuniamini. Pia nimepata salaam nyingi za kunimiss kwenye game kutoka kwa mashabiki wangu wengi sana kutoka kona mbalimbali za dunia hii. Ni kweli kabisa kwamba kwa sasa nina majukumu makubwa sana ya kuwatumikia wananchi wenzangu wa jimbo la Mikumi lakini hilo halisababishi mimi kushindwa hata kwa uchache kuendelea kufanya muziki na kuwatendea haki mashabiki wangu wa ukweli walionibeba tangu siku ya kwanza mpaka sasa wanaendelea kuwa pamoja sana na mimi, ikumbukwe mimi ni mwanamuziki na nitaendelea kuwa mwanamuziki mpaka nione kibao kimeandikwa hakuna muziki”. Alisema Prof Jay

Mbali na hilo Prof Jay amefunguka na kusema muziki kwake ndiyo ulifungua njia katika maisha yake na leo kumfanya kupata heshima kubwa kwa watanzania hususani kwa watu wa Mikumi kama mbunge wao, kutokana muziki ambao alikuwa akifanya.

“Muziki umenilea, muziki umeendesha maisha yangu na familia yangu, muziki ndio ulionipa heshima kubwa sana ulimwenguni, bila muziki leo nisingekuwa mbunge wa Mikumi. Nawaahidi mashabiki wangu wote mliokuwa mnaniuliza mara kwa mara kama nimeacha kufanya muziki kuwa nitaendelea kufanya muziki till i die, maana hiki ni kipaji cha hali ya juu nilichopewa na Mungu kwa makusudi na kwa Upendeleo mkubwa na sio kwa bahati mbaya. Nimewasikia na muda sio mrefu nitawatendea haki, ahsanteni sana kwa kuniamini nawapenda sana, huu ni mgodi unaotembea” Prof Jay

EATV.TV

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364